Psalms 140

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)


1 aEe Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu;
nilinde na watu wenye jeuri,

2 bambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao,
na kuchochea vita siku zote.

3 cWao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,
sumu ya nyoka iko midomoni mwao.


4 dEe Bwana, niepushe na mikono ya waovu;
nilinde na watu wenye jeuri
wanaopanga kunikwaza miguu yangu.

5 eWenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,
wametandaza kamba za wavu wao,
wametega mitego kwenye njia yangu.


6 fEe Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”
Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.

7 Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,
unikingaye kichwa changu siku ya vita:

8 gEe Bwana, usiwape waovu matakwa yao,
usiache mipango yao ikafanikiwa,
wasije wakajisifu.


9 hVichwa vya wanaonizunguka vifunikwe
na shida zinazosababishwa na midomo yao.

10 iMakaa ya mawe ya moto na yawaangukie!
Na watupwe motoni,
katika mashimo ya matope,
wasiinuke tena kamwe.

11 jWasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;
maafa na yawawinde watu wenye jeuri.


12 kNajua kwamba Bwana huwapatia maskini haki,
na kuitegemeza njia ya mhitaji.

13 lHakika wenye haki watalisifu jina lako,
na waadilifu wataishi mbele zako.
Copyright information for SwhKC